Wilaya ya Kalambo ilianzishwa rasmi Julai 01, 2012 kwa tangazo la Serikali (GN 72) na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ilianzishwa tarehe 23 Desemba, 2012 kwa kumegwa toka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na kutangazwa kuwa Halmashauri Mwezi Januari 2013 kwa tangazo la Serikali (GN 631). Halmashauri ilianza kutekeleza Bajeti yake rasmi kuanzia tarehe 01 Julai 2013.
Wilaya ya Kalambo ina eneo la kilometa za mraba 4,715. Kati ya hizo kilometa za mraba 504 ni za maji na kilometa za mraba 4,211 ni za nchi kavu.
Makao Makuu ya Wilaya yapo katika Mji wa Matai umbali wa kilometa 52 kutoka Makao ya Mkoa wa Rukwa. Wilaya hii ina Jimbo 1 la Uchaguzi, Tarafa 5, Kata 23, vijiji 111 na vitongoji 439.
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Kalambo ina watu 207,700 kati yao Wanaume wapo 100,474 na Wanawake wapo 107,226. Kwa mwaka huu 2016 Wilaya hii inakadiriwa kuwa na watu 238,760 ambapo wanawake wanakadiriwa kuwa 123,261 na wanaume 115,499.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.