Kusimamia na kutoa mapato toka vyanzo vya mapato vya Halmashauri, Serikali kuu, Wahisani na Wafadhili mbalimbali
Kulipa malipo kwa wateja mbalimbali ikiwa ni pamoja na watumishi, Taasisi mbalimbali, wazabuni na wateja wanaotoa huduma kwa Halmashauri.
Kuandaa Taarifa za Mapato na Matumizi kwa kila mwezi, robo, nusu na mwaka mzima na kuzipeleka Hazina, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, kwa Katibu Tawala na sehemu nyingine zinakohitajika.
Kuhakikisha vitabu vya Halmashauri vinaandaliwa na kuandikwa kwa umakini, na taarifa za mapato na malipo zinaandikwa kila siku katika vitabu.
Kuandaa taarifa za usuluhishi wa Benki kila mwezi
Kujibu hoja za ukaguzi wa ndani wa hesabu na hoja za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali, pia kujibu hoja za ukaguzi zitokanazo na Mkaguzi wa mfuko wa barabara, mfuko wa pamoja (Basket Fund) na mpango wa maendeleo ya elimu.
Sekta ya Biashara
Kuainisha masoko ya bidhaa zinazopatikana katika Halmashauri
Kuhakiki ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa katika Halmashauri
Kusimamia sheria za biashara Na.25 ya mwaka 1972, Na Sheria ya vileo Na.28 ya mwaka 1968 na sheria ya ushuru wa nyumba za kulala wageni (Hotel levy act) Na.23 ya mwaka 1973.
ushauri na usimamizi wa Biashara na uwekezaji katika Halmashauri.