Mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 60 jela Crement Salama mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa kata ya Kasanga wilayani kalambo kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba miaka 17 kisha kumpatia ujauzito.
Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi wilayani humo Mlisho Kimbeho, amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo April 2020 kisha kufikishwa mahakamani kwa makosa mawili, la kwanza ikiwa ni kumbaka mwanafunzi na lapili ikiwa ni kumpatia ujauzito mwanafunzi huyo.
Hata hivyo baada ya mahakama hiyo kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha, mshitakiwa alikiri wazi kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani ni kijana mdogo ambaye bado ni tegemezi.
Awali akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Ramadhan Rugemalira, amesema mtuhumiwa alitenda kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha sheria 130 (1) 2e na kifungu cha 131( 1) cha sheria kanuni ya adhabu kwa kumbaka mwanafunzi kisha kumpatia ujazito na kumsababishia kuto endelea na masomo yake. Na kusema Hivyo mahakama inamuhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 60 jela.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.