Mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imemhukumu kwenda jela miaka thelathini Medadi Chitenzi mmbambwe miaka 55 mkazi wa kijiji cha Ulumi ‘A’’wilayani humo, baada ya kupatikana na kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 10 .
Mtuhumiwa alishitakiwa kwa kosa hilo alilo daiwa kulitenda kinyume sheria na kifungu 130(1) na (2)(e) na131(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019. Ambapo mshitakiwa alitenda Kosa hilo tarehe 12/08/2020 katika kijiji cha Ulumi "A" wilayani humo ,ambapo ilielezwa mahakamani hapo mtuhumiwa alitenda kosa hilo wakati akiwa amelewa.
Hata hivyo mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashitaka ukawa na jukumu la kuthibitisha bila shaka tuhuma zinazomkabili mshitakiwa,ambapo upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Rajabu Ndunda ulitafuta ushahidi kwa kutoa vilelezo vilivyopelekea mshitakiwa kukili kosa lake na kuiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani alitenda kosa hilo bila kukusudia kutokana na kuwa alikuwa amelewa.
Kwa kuzingatia maombi ya msitakiwa na maombi ya mwendesha mashitaka, hakimu wa wilaya hiyo Nicsoni temu,amemuhukumu mshitakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kola la kumbaka mtoto huyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.