- Serikali kupitia wizara ya mali asili na utalii hapa nchini imeshauriwa kuwekeza zaidi kwenye maporomoko ya kalambo falls yalipo mkoani Rukwa kwa kuyatangaza na kuweka miundombunu rafiki ambayo itasaidia kuongeza idadi kubwa ya watalii kutoka ndani na nje ya nchi kutembelea maeneo hayo kwa wingi na hatimaye kuongeza pato la taifa.
Maporomoko ya Kalambo falls ni ya pili afrika kwa urefu kutoka maji yanapoanzia kumwagika hadi yanapodondokea kwa mita 235na upana wa mita 3.6 hadi mita18, licha ya maporoko hayo kuwa naurefu na kuwa kivutio kikubwa kwa watalii bado kumekuwa na changamoto ya miundombinu kuto boreshwa ikiwemo barabara pamoja na sehemu za kufikia wageni.
Badhi ya watalii wa ndani kutoka hapa nchini wametembelea maporomoko hayo na kuishauli serikali kupitia wizara ya mali asili na utalii kuanza kufikiria kuwekeza zaidi katika maaeneo hayo kutokana na maporomoko hayo kuwa kivutio kikubwa kwa afrika na dunia kwa ujumla.
Fransista Makoe kutokaTamisemi idara ya usitawi wa jamii amesemaendapo serikali ikiwekeza kwa kwa kiwangokikubwa katika maeneo hayo mapato yatapatikana na kusaidia kuhudumiajamii.
Kwa upande wake show Nshurume kutoka nchini Swaziland amesema amevutiwa na maporomoko hayo kutokana na maeneo hayo kuwa mazuri nayanayo vutia na kuwasihi watu wengine kufika kwenye maeneo hayo iili kuona madhari yake.
Mkurugezi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kalambo Msongera Palela amewataka wananchi kujenga mazoea kutembelea vivutio vya ndani hususani katika maporomoko hayo ambayo ni ya pili Afrika kwa urefu.
‘’Nimefika na wageni hawa lengo ikiwa ni kuwaonesha kileamcho kipo kwenye maeneo hayo kwani mazingira mazuri yenye maporomoko yanayovutia kwa kila sehemu hivyo ningewasihi wananchi kuendelea kufika kwenye maeneo haya ili kujiuonea majabu ya mwenyezi mungu’’alisema palela
Aidha amesema kwa kutambua umuhimu wa maromoko hayo serikali kupitia wakala wa huduma za uhifadhi wa misitu Tanzania TFS imeanza kufanya marekebisho ya miundombinu kwa kujenga hotel pamoja na ngazi za kushikia kwenye maeneo husika.
Hali kadharika endapo wananchi wakiendelea kujengamazoea ya kutembelea vivutio mbalimbali vilipo hapa nchini sambamba na kuvitangaza serikali itapata mapato mengi sambamba na watalii kutoka nje ya nchi kuongezeka maradufu.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.