Serikali mkoani Rukwa imekamilisha ujenzi shule mpya 12 za msingi na sekondari ambazo zimejengwa kwa thamani ya shilingi billion 6.064 na kuwawesha wanafunzi wa darasa la kwanza 30.922 sawa na asilimia 60.2 Kuanza masomo ya elimu ya msingi
Mapema akiongea ofisini kwake mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amesema kwa upande wa Darasa la awali mkoa ulilenga kuandikisha Wanafunzi 57,006 kati yao jinsia ya kiume wakiwa 27,885 na jinsia ya kike wake wakiwa 29,121) ambapo hadi kufikia tarehe 04 Januari, 2024 Wanafunzi 24,033 wa Darasa la awali sawa na asilimia 42.1 walikuwa wameandikishwa kuanza darasa la awali.
‘’ Kwa upande wa Darasa la kwanza Mkoa ulilenga kuandikisha Wanafunzi 51,347 kati yao jinsia ya kiume wakiwa 25,254 na jinsia ya kike wakiwa 26,093) ambapo Mpaka tarehe 04 Januari, 2024 Jumla ya Wanafunzi 30,922 walikuwa wameandikishwa kujiunga na darasa la kwanza sawa na asilimia 60.2’’. alisema Makongoro.
Aidha amesema Kwa upande wa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu Jumla ya Wanafunzi wa Darasa la awali 167 kati yao jiansia ya kiume wakiwa 69 na wakike 98) wameandikishwa na kwa upande wa Darasa la kwanza kwa Wanafunzi wenye Mahitaji maalum jumla ya Wanafunzi 91, wameandikishwa.
Hata hivyo Jumla ya Wanafunzi 31,182 waliofanya mtihani wa kuhitimu darasa la Saba mwaka 2023, kati ya hao Wavulana walikuwa 13,946 na Wasichana 17,236 sawa na asilimia 97.2 baada ya matokeo ya Mtihani Jumla ya wanafunzi/watahiniwa 24,415 wakiwemo wavulana 11,270 na wasichana 13,145 walifaulu sawa na asilimia 78.30 na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.