Baraza la madiwani katika halmashauri ya Kalambo Mkoani Rukwa limepitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti ya shilingi 34,060,221,000.00 huku shilingi 2,412,405,000.00 zikitarajiwa kutoka kwenye mapato ya ndani na shilingi 10,839,724,000 ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.
Wakiongea wakati wa upitishaji wa mpango wa bajeti hiyo madiwani katika halmshauri hiyo wamemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kuboresha vyanzo vya mapato pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani ili kufikia maelengo ya serikali katika ukamilishaji miradi ya maendeleo ikiwemo maboma ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi.
Awali akiongea kupitia kwenye baraza hilo mkurugenzi mtendaji wa halmshauri hiyo Shafi Mpenda amesema bajeti hiyo imezingatia ukamilishaji wa miradi ilioanzishwa kwa nguvu za wananachi pamoja na uboreshaji wa vyanzo vya mapato ikiwemo minada ya mifugo na kuwataka madiwani kushirikina kwa karibu na timu za mapato ili kufikia malengo ya serikali katika kuwahudumia wananachi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.