BARAZA la madiwani wilayani Kalambo mkoani Rukwa limeazimia kuwafukuza kazi ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Takukuru watendaji wote wa serikali za vijiji waliohusika kuiba fedha za makusanyo ya mapato ya ndani kiasi cha shilingi milioni120.5 na kuzitumia katika matumizi yao binafsi huku baraza hilo likitoa siku 30 fedha hizo kurejeshwa.
Kwa kipindi kuanzia Julay hadi aprily 2020 Halmashauri ya Kalambo imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi billion 1.14 sawa na asilimia 61.87, lakini changamoto kubwa kwa hivi sasa ikitajwa kuwa ni baadhi ya shughuli za maendeleo kukwama kutokana na watendaji kula fedha za makusanyo kiasi cha shilingi million 120.5.
Diwani kata ya Mkoe Alfred Mpandashalo, alisema mpaka sasa watendaji hao wamekuwa wakijikopesha fedha kinyume na utaratibu na kujikuta wakidaiwa madeni makubwa ambayo hata kuyalipa inakuwa kazi kubwa kwao.
Alisema ili kuweka fundisho ni muhimu watendaji wote wakachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Diwani wa kata ya Kisumba Inosent Lungwa, alisema kila diwani anawajibu wa kuwabana watendaji kupitia maeneo yao husika kabla ya kula fedha na kusema hali hiyo imekuwa ikijitokeza kutokana na kutokuwepo kwa mkakati wa kuwabana watumishi hao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kalambo Daud Schone , alisema kupitia kikao cha mipango na fedha walikukubalina kuwafukuza kazi watendaji wote ambao watashindwa kurejesha fedha hizo.
Alisema mpaka sasa baadhi yao wamepelekwa Takukuru ili kujibu tuhuma zinazo wakabili na wamewekewa muda maalumu wa kuzilipa fedha hizo.
“nguvu yetu tulio nayo kwa hivi sasa ni kuwafukuza tu ,kwani watendaji hao sasa wamekuwa ni sugu. pia katika kikao chetu cha tuilikubalina kuwafukuza watendaji wote ambao watashindwa kulifa fedga hizo. Alisema Sichone.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo, alimwagiza mkurugenzi kuhakikisha anaimarisha usimamizi wa ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo na kusisitiza ukaguzi wa ndani kutumika kikamilifu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika miradi yote .
Alisema Halmashauri inatakiwa kuhakikisha kuwa makusanyo yote ambayo hayakupelekwa benk yanapelekwa na pia kuzingatia agizo la 50 (5) la memoranda ya fedha za serikali za mitaa ya mwaka 2009 linaloeleza makusanyo yote ya mapato kupelekwa benk kabla ya kutumika.
“Halmashauri yenye uwezo mzuri wa ukusanyaji mapato ndiyo inaweza kutekeleza kikamilifu wajibu wake wa utoaji huduma na utekelezaji wa miradi ikiwa ni pamoja na kuongoza usitawi wa maisha ya wananchi” alisema wangabo.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa katika mwaka wa fedha wa 2018 / 2019 watendaji wapatao 14 walifukuzwa kazi na baraza hilo kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo za wizi wa fedha za mapato
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.