Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) wilayani Kalambo mkoani Rukwa imeanza ujenzi wa mradi wa miundombinu ya kutibu maji katika milima ya Singiwe kata ya Lyowa utakao gharimu fedha kiasi cha Shilingi 1,623,031,819 hatua itakayo wezesha wananchi kuondokana na adha ya kutumia maji yaliyo changanyikana na tope wakati wa msimu wa mvua za masika.
Kaimu meneja wa wakala ya maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) wilayani humo ndugu Francis Mapunda, amebainisha kuwa mradi huo utatekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja na kwamba lengo ni kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya kutumia maji yaliochanganyikana na tope wakati wa msimu wa masika.
Aidha amebaimisha kuwa huduma ya upatikanaji wa maji wilayani humo imeongozeka kwa asilimia 81 ambapo vijiji 83 kati ya vijiji 111 vimepata huduma ya maji.
Baadhi ya wananchi wilayani humo ambao licha ya kuipongeza serikali kwa hatua hiyo wameomba mradi huo kuharakishwa ikiwa ni pamoja na kudhibiti wananchi wanaoendesha shughuli za kibinadamu kando ya mito ikiwemo kilimo na mifugo kwenye vyanzo vya maji.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.