• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

BILIONI 3.8 KUJENGA MADARASA 191 RUKWA- RC SENDIGA..

Posted on: October 20th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amesema atahakikisha fedha zote zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya 191 kwenye shule za sekondari mkoani humo zinatumika kama ilivyokusudiwa ili wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023 waweze kuanza masomo yao kwa wakati.

Serikali ya Awamu ya Sita imeupatia mkoa wa Rukwa shilingi Bilioni Tatu na Milioni Mia Nane na Elfu Ishirini (3,820,000,000/-) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa katika halmashauri nne za mkoa wa Rukwa ambapo kila darasa litajengwa kwa shilingi Milioni Ishirini kupitia mfumo wa “Force Account”.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (03 Oktoba,2023) ofisini kwake mjini Sumbawanga Mhe. Sendiga alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha wanafunzi wote wanapata mahala bora na salama kusomea.

“Natoa wito kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kufuatilia kwa ukaribu ujenzi wa madarasa hayo ili yaweze kukamilika kwa muda yaani ndani ya siku Sabini na Tano (75) kama alivyoelekeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI na kwa ubora ulioelekezwa pamoja na kukamilisha utengenezaji wa madawati yake” alisisitiza Sendiga.

Katika taarifa yake, Mhe. Sendiga alisema mkoa umefanya maoteo  ya  Wanafunzi 26,655 wa kujiunga Kidato cha kwanza mwezi Januari, 2023.  Maoteo hayo ni kutoka jumla ya watahiniwa 33,319 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya msingi mwaka 2022 sawa na asilimia 80 ya ufaulu ambapo wanafunzi hao watahitaji jumla ya madarasa 534 ambapo madarasa yaliyopo ni 343  na upungufu ni madarasa 191.


Sendiga alitaja  mchanganuo wa idadi ya  vyumba 191 vya madarasa kwa kila Halmashauri kwenye mabano, Manispaa ya Sumbawanga  (56)  sawa na shilingi  1,120,000,000/= ,Halmashauri ya  Nkasi (26)  sawa na shilingi  520,000,000/= Halmashauri ya Sumbawanga (46)  sawa na shilingi 920,000,000/= na Halmashauri ya Kalambo (63) sawa na shilingi 1,260,000,000/=.                         Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kalambo Tano Mwela ,amesema atahikikisha fedha hizo zinatumika kulingana na malengo ya Serikali.


Mwisho.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.