Katika jitihada za kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi katika mazingira mazuri na wezeshi baraza la wafanyakazi katika Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa limepitisha mpango wa mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kiasi cha shilingi 3,063,730,000.00 kwa ajili ya kulipa madai mbalimbali ya watumishi na jumla ya shilingi 1,420,618,000,0 ikiwa ni kwa ajili ya watumishi 661 watakao panda madaraja.
Licha ya hilo baraza hilo limepitisha mapendekezo ya bajeti ya shilingi 1,643,112,000.00 kwa ajili ya watumishi 1,218 watakao pata nyongeza ya mishahara, ambapo jumla ya shilingi 481,040, 000, zimetengwa kwa kila Divisheni na vitengo kwa ajili ya kulipa likizo,uhamisho na madeni mbalimbali kwa watumishi wa umma.
Awali akifungua kikao cha baraza hilo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya jamii Wambura Sundy alitumia fursa hiyo kuwataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo ya serikali.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.