Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa kimeuhakikishia umma kuwa kitashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na utekelezaji sahihi wa ilani yake ya uchaguzi huku kikiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha na kupiga kura ifikapo 24 Novemba kuwachagua viongozi bora kwa maendeleo ya Taifa.
Wilaya ya Kalambo yenyeVitongoji 422, Vijiji 111, kata 23 na Tarafa 4 ambazo ni Kasanga, Matai, Mwimbi na Mambwe, inakadiriwa kuwa na jumla ya watu 271,393 wakiwemo wanaume 131,285 na wanawake 140,108 ambao wote wanatakiwa kuhamasishwa vilivyo ili washiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu.
Katibu wa Siasa na Uenezi Wilayani Kalambo John Mbita amesema chama kimejidhatiti vilivyo kuelekea kwenye ushindi kwani Mwenyekiti wa chama hicho kitaifa Mh. Rais Wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania Dr,John Pombe Magufuli ametekeleza kwa asilimia mia moja ahadi zote.
‘’Kila mwananchi ana haki sawa ya kugombea na kupiga kura, kama mwana Falisafa mkongwe wa Marekani kutoka Chuo Kikuu cha Havard Profesa John Luke kupitia nadharia yake ya uwakilishi [Represantation theory]. Hivyo wananchi wote tujitokezeni kwa wingi katika kujiandikisha na kupiga kura kwani ni haki yetu ya msingi ifikapo tarehe 24 Novemba 2019 ili tupate viongozi bora watakao tuletea maendeleo.’’Alisema Mbita
Wakiongea kupitia maadhimisho ya uzinduzi wa ligi ya mapinduzi Cup yaliyofanyika katika kata ya Mwazye Wilayani humo,viongozi na makada wa chama cha mapinduzi CCM, wamesema kimsingi kila mwananchi anahaki ya kugombea na kupiga kura.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.