Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa kimewataka vijana kujenga mazoea ya kushiriki kwenye michezo mbalimbali ambayo imekuwa ikianzishwa na wadau kwa lengo la kuwasaidia kuimarisha afya zao na kujiajiri wenyewe.
Kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya vijana kushindwa kushiriki kwenye michezo ambayo imekuwa ikianzishwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa na hivyo kupelekea Chama cha Mapinduzi wilayani humo kuchukua hatua ya kuanzisha ligi ambayo itashirikisha zaidi ya timu sita katika Tarafa ya Mwazye wilayani humo.
Akizindua michezo hiyo Katibu wa itikadi, siasa na uenezi wilayani humo John Mbita, amesema lengo la michezo hiyo ni kuhakikisha vijana wanashiriki kikamilifu kwenye michezo
‘’Chama cha Mapinduzi kata ya Mwazye kimekusudia kwa nia ya dhati kuanzisha ligi ya kipekee yenye kuunganisha jamii kwa masilahi mapana ya jamii nzima ikiwemo kufungua fulsa ya michezo kama ajira kwa vijana na kukuza vipaji kwa kuwatangaza nje na ndani kupitia vyombo vya habari’’ alisema Mbita.
Amesema dira kuu ya fainali ya mapinduzi cup mwaka huu ni kuunda timu ya kata yaani combined team na kuiwezesha kushiriki ligi kubwa za kiwilaya na mkoa pia.
Katibu wa vijana wa Chama cha Mapinduzi, CCM wilayani humo Peter Monko, amesema vijana wanatakiwa kushiriki kwenye michezo kwa lengo la kuwasaidia kujiajiri pamoja na kuimarisha afya zao.
Kata ya Mwazye inaundwa na matawi manne ya CCM, ambayo ni Kazila,nMwazye, Msoma na Mpenje. Hivyo ligi ya mapinduzi inajumuisha timu nne ambapo kila kijiji kimetoa timu moja kwa kingilio cha shilingi elfu thelathini (30,000/=).
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.