Katibu tawala wilayani Kalambo Mkoani Rukwa Frank Sichalwe amekabidhi pikipiki 7 kwa watendaji wa kata ambazo zitasaidia katika shughuli za ukusanyaji wa mapato pamoja na kuwafikia wanafunzi ambao wameshindwa kuripoti shule tangu kuanza kwa msimu wa mhula mpya wa masomo Januari 9/2023
Aidha kupitia hafla hiyo Sichalwe aliwataka watendaji kuzitumia pikipiki hizo kulingana na malengo ya serikali ikiwemo kuwafikia wananchi na kutatua kero zao kwa wakati
Mapema akiongea kupitia hafla hiyo mhazini wa wilaya hiyo Patrick Msafi amesena licha ya hilo halmashauri ina mpango wa kuongeza pikipiki zingine 16 ambazo zitasaidia katika kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato vijijini na kusema hadi sasa halmashauri imefikia asilimia 56 ya ukusanyaji mapato
Mwenyekiti wa watendaji wa kata wilayani humo John Benson ambaye pia ni mtendaji wa kata ya Katete aliipongeza serikali kwa kuwapatia msaada huo na kusema pikipiki hizo zinaenda kuwasaidia katika kupunguza gharama za usafiri
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.