Uongozi wa serikali wilayani Kalambo mkoa wa Rukwa umewaagiza watumishi wote wa umma wilayani humo kusajili laini za simu zao za mitandao mbalimbali kwa njia ya alama za vidole ili kuimarisha utendaji wao bora wa kazi.
Akizindua zoezi la mkakati wa kusajili laini za simu wilayani kalambo katibu tawala wilayani wilayani humo Frank Sichalwe, amesema usajili huo utawawezesha watumishi hao kutoa huduma inayostahili kwa wakati unaostahili na kusaidia kuchochea shughuli za maendeleo ya jamii.
Amesema zoezi hilo litatawahusu watu wote kutoka maeneo ya vijijini na mijini na kusema kwa sasa wameanza na watumishi wote wilayani humo kwa kupatia elimu.
Baadhi ya wakazi wa mji mdogo wa matai wilayani kalambo mkoa wa Rukwa wameelezea umuhimu wa kusajili laini za simu kwa njia ya alama za vidole na kusema utaratibu huo utalinda usalama wa mteja kutokea uwezekano wa kufanyiwa vitendo vya uhalifu na watu wenye nia ovu.
Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano-tcra- kanda ya nyanda za juu kusini mhandisi Asajile John, amesema lengo la serikali katika kutekeleza zoezi hili ni kutoa wigo mpana wa kuthibiti uhalifu wa mtandaoni na kuthibiti matumizi mabaya ya simu .
Kawie Ntemo afisa usajili wa vitambulisho vya nida wilayani kalambo amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa kujisajili ilikmupata vitambulisho vya uraia kwa lengo la kuondokana na matatizo yasio kuwa ya lazima.
mamlaka ya mawasiliano-tcra- kanda ya nyanda za juu kusini inaendesha zoezi la kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole katika mikoa ya Rukwa na Katavi kabla ya ukomo wa zoezi hili mwezi december mwaka huu
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.