Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Julieth Binyura amepiga marufuku wavuvi wa mwambao wa ziwa Tanganyika kuuza samaki zao katika nchi za jirani na kuelekeza samaki zote kupelekwa katika masoko madogo wakati wakisubiri kusogea mbali kwaa maji ya ziwa Tanganyika baada ya kulizingira soko kuu la samaki lililoko katika mji wa Kasanga.
Hatua hiyo inakuja baada ya kujitokeza malalamiko kutoka kwa wavuvi juu kukosa sehemu ya kuuzia samaki zao baada ya soko kuu la samaki Kasanga kuzingirwa na maji ya ziwa Tanganyika na kupelekea kufungwa kwa soko hilo kwa muda usiojulikana.
Ameyasema hayo baada ya kufanya ziara kwenye vijiji vyote vya mwambao kukagua miundo mbinu,uvuvi haramu na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
,,Acheni kuuzia samaki Zambia. Naomba mzihifadhi zikauke kwani baada ya muda mfupi maji yaliyozingira soko letu la Kasanga yatasogea mbali na kuliacha soko likiwa huru tayari kwa biashara kufunguliwa.
‘’Wavuvi wote tumieni nyavu zilizo ruhusiwa kwani hatutaki mfirisiwe kwa kuwa baada ya kuwakamata tutawapeleka mahakamani na kutaifisha vyombo vyote vya uvuvi.”Amesisitiza Binyura.
Mapema mwaka juzi, Mkuu wa Wilaya hiyo aliongoza zoezi la uchomaji nyavu haramu na kuwaonya wavuvi kuacha kabisa tabia hiyo kwani inaathiri uzao wa samaki na ni uvunjaji wa sheria zinazo simamia masuala ya uvuvi nchini Tanzania na duniani kote.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.