Mkuu wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura amewataka wazazi na walezi mkoani Rukwa kuwalea watoto wao katika malezi bora na kujiepusha na vitendo vya ukatili ikiwemo vipigo sambamba na kujiepusha na migogoro ya kifamilia ambayo imekuwa ikijitokeza na kusababisha tatizo la watoto wa mitaani.
Chimbuko la haki za mtoto lilitokana na mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto ulioidhinishwa na Nchi wanachama wa umoja wa mataifa mnamo novemba 20,1989 na kuridhiwa na serikali ya jamhuri ya mungano wa Tanzania Juni10,1991.
Hata hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa haki za watoto umoja Afrika ulipitisha mkataba wa afrika wa haki na usitawi wa mtoto mwaka 1990 na huku mkataba huo ukilenga kuhakikisha kuwa mkataba wa kimataaifa wa haki za mtoto unatekelezwa kwa kuzingatia mila ,desturi,na tamaduni za kiafrika .
Kwa ujumla mikata yote miliwili ililenga kutoa majukumu kwa serikali zinazoridhia kulinda na kuendeleza haki za mtoto ili kutekeleza mikataba hiyo ambapo serikali ya jamhuri ya Tanzania iliandaa sera ya maendeleo ya mtoto 2008 na kutenga, na kutunga sheria ya mtoto Na21 ya mwaka 2009 na kanuni zake ilikuweza kutekeleza haki hizo mihimu.
Akizindua mradi wa kutambua haki za watoto uliokuwa umeandaliwa na shirikia la Future and Hope-(BETHANIA HOMES), mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura amesema wazazi na walezi wanatakiwa kuhakikisha watoto wao wanaendelezwa katika nyanya za kielimu,kimaadili,na kiimani.
‘‘niwasihi wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanapewa nafasi ya kushiriki na kushirikishwa katika masuala yanayowahusu ikiwa ni pamoja kutoa maoni ,kusikilizwa na kushiriki katika maamuzi mbalimbali katika familia na jamii kwa ujumla ‘’alisema Binyura.
Amesema katika sheria ya mwaka 2009 mtoto anahaki mbalimbali katika jamii ikiwemo kupata haki ya kuishi,kupumzika kuheshimiwa na kuthaminiwa.
Joseph Kasaila mratibu wa tasisi ya Future and Hope –BETHANIA HOMES,amesema wamelazimika kupeleka mradi huo utahudumu katika eneo la Matai wilayani kalambo na kusema lengo kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata ulewa juu ya umuhimu wa kuwalea watoto kwa lengo la kupunguza wimbi la watoto wa mitaani.
‘’mfano watoto wanao pitia adha hiyo ni wanaopitia hali hii ni wale ambao waliofiwa na wazazi wote wawili(yatima) watoto wanaohusishwa na huduma za kingono kinyume na sheria ,watoto wanaofanya kazi mogodini ,watoto wanaokinzana na sheria ,watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ,watoto wenye ulemavu na watoto wenye mambukizi ya VVU na UKIMWI.’’alisema Kasaila
Kaimu kurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo yasita Nkyabonaki , amesema kila mzazi anatakiwa kuhakikisha waatoto wanalelewa katika misingi bora na tabia njema.
‘’marekebisho yanaanziakatika ngazi ya familia na jamii ,ambapo wazazi /walezi na wanajamii wanajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa kila mtoto analelea na kukua kwa kufuata maadili,mila ma destruri za jamii husika.’’alisema Nkyabonaki.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.