Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Kalambo kusitisha utolewaji wa vibari vya kuingiza mifugo katika kijiji cha Madibila kutokana kijiji hicho kuwa na mgogoro kati ya wafugaji na wakulima uliosababisha baadhi wafugaji kupigwa na kuumizwa kutokana na kulisha na kupitisha mifugo kwenye mazao ya wakulima.
Ameyasema hayo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mabidila wilayani humo na kusisitiza kila mfugaji kutumia eneo lake katika kulisha mifugo yake.
Alisema kuwa mfugaji ni lazima aitathimini idadi ya mifugo aliyonayo ukilinganisha na eneo lake la malisho alilonalo na kuwa kwa kufanya hivyo watapunguza migogoro kati yao na wakulima.
Mkuu huyo wa wilaya alitaka Halmashauri kuweka utaratibu mzuri kupitia serikali za vijiji kutopokea mifugo mipya toka kwa wafugaji kama watakua hawana maeneo ya kutosha ya kuchungia.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Nicholaus Mlango aliunga mkono kauli hiyo ya mkuu wa wilaya na kuwataka wafugaji kufauata taratibu za uingizaji mifugo kwenye maeneo ya vijiji ili kuepuka migogoro.
Mmoja kati ya Wananchi ambaye ni mkulima Sande Sichilima alidai kuwa kama agizo hilo la serikali la kusitisha vibali vya kuingiza mifugo katika vijiji litatekelezeka imani yake ni kuwa migogoro itatoweka kabisa.
Alisema kuwa katika kijiji Madibira mifugo imekuwa mingi ukilinganisha na eneo la malisho na ndiyo maana migogoro imeanza kujitokeza na kuishukuru serikali kwa hatua hiyo iliyoichukua ya kusitisha vibali vipya vya kuingiza mifugo katika wilaya hiyo.
Ntinga Luhende ambaye ni mmoja wa Wafugaji alidai kuwa wao wamepokea maamuzi ya serikali na watahakikisha mifugo mipya aipelekwi katika wilaya ya Kalambo hususani kijiji cha Madibira
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.