Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Dkt. Lazaro Komba amesema Serikali imetoa mashine tano (5) kwa ajili ya kuchanganya virutubishi vya vyakula kwa ajili ya wanafunzi shuleni ambavyo vitasaidia kuimarisha afya na kufikia hali stahimilivu ya ukuaji wa mwili na akili.
Ameyasema hayo kupitia kikao cha taarifa za utekelezaji wa Afua za Lishe robo ya kwanza kwa mwaka 2025/2026 na kusisitiza Watendaji wa Kata kusimamia zoezi la utoaji vyakula shuleni ikiwemo kuweka akiba itakayo wezesha wanafunzi kupata chakula wakati wote.
Aidha, amewaagiza Watendaji wa Kata pamoja na Waratibu wa Afua za Lishe kusimamia kwa ukaribu zaidi uanzishwaji wa mashamba darasa ikiwemo mashamba ya mboga mboga na matunda ambayo yatasaidia wanafunzi kuepukana na tatizo la udumavu na utapia mlo mkali na kuimarisha Afya zao wakati wote wawapo shuleni.
Hata hivyo kiwango cha wanafunzi wanao kula shuleni kimeongezeka kutoka asilimia 85% ya robo ya nne kwa mwaka 2024/2025 hadi kufikia asilimia 89.84 kwa robo ya kwanza kwa mwaka 2025/2026.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.