Mkuu wa wilaya Ya kalambo mkoani Rukwa Lazaro komba ameyataka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali NGO’S yanayotekeleza miradi mbalimbali wilayani humo kuzitumia fedha za ufadhili katika kutekeleza miradi ambayo haikinzani na mila, maadili na Desturi za utamaduni wa Mtazania.,
Ameyasema hayo kupitia kikao cha robo ya kwanza na viongozi wa mashirika yasio kuwa ya kiserikali na kuwakilishwa na afisa tawala wilayani humo Oktavian Show na kusisitiza mashirika hayo Kutumia ufadhili kwa kuzingatia dhamana ya fedha katika miradi inayosaidia jamii na siyo kutumia fedha hizo kwa ajili ya gharama za uendeshaji
Aidha akasisitiza Kutoa taarifa za fedha, vyanzo vya mapato na matumizi ya rasilimali kila robo mwaka kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Halmashauri kwa msajili msaidizi wa NGOs.
Mapema akiongea kupitia kikao hicho Kaimu mkurugenzi wa halmshauri hiyo Sunday Wambura akasisitiza NGOs kufanya kazi kwa mujibu wa nyaraka zao za usajili na si vinginevyo kama ilivyoelekezwa na kifungu cha 30(20) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na 24 ya Mwaka 2002.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.