Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba amewataka wananchi wilayani humo kujenga mazoea ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa ujenzi kabla ya kuanza shughuli za ujenzi ili kuepuka madhara ya nyumba kubomoka na kuezuliwa na upepo.
Hatua hiyo inakuja baada ya baadhi ya maeneo hivi karibuni wilayani humo, mvua kuezua na kubomoa nyumba za wananchi na kuwasababishia hasara. Ambapo amewataka kujenga mazoea ya kujenga nyumba imara na kwa saruji na kupanda miti ya kutosha kwenye maeneo ya makazi ili kuepuka madhara ya nyumba kuezuliwa kila mwaka.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.