Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba amewataka wananchi wilayani humo kutunza mazingira na kuacha kulima kando ya vyanzo vyamaji ili kuepuka ukame.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi ccm wilayani humo wakati wa ukaguzi miradi ya maji katika kata za Kasanga na Kisumba na kusisitiza jamii kutunza miundombinu ya maji na kuacha kuendesha shughuli za kilimo kando ya vyanzo vya maji.
Mapema akiongea kupitia ukaguzi miradi hiyo mwenyekiti wa ccm wilayani humo Vitusi Nandi amesema lengo la serikali ni kuwawesha wananchi kupata huduma ya maji karibu na maeneo yao husika na kusisitiza miradi hiyo kulindwa na kumtaka meneja wa Ruwasa wilayani humo kuunda vyombo vya watumiaji maji ambavyo vitafanya miradi hiyo kuwa endelevu.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.