Mkuu wa wilaya ya Kalambo Tano Mwela ametoa wito kwa wananchi kuwalinda watoto dhidi ya maafa ya mvua ambayo yamekuwa yakijitokeza na kusababisha vifo vyao.
Aliyasema hayo wakati akitoa misaada ya kibinadamu kwa wananchi waliokuwa wamepatwa na maafa ya mvua katika kijiji cha Charaminwe wilayani humo iliokuwaimenyesha katika milima ya Singiwe na kusababisha vifo vya watoto wanne kufariki dunia baada ya kusombwana na maji na kusisitiza wazazi na walezi kujenga mazoea ya kuwalinda watoto wao kwakuhakikisha wanapelekwa shule ili kutimiza ndoto zao za badae.
Licha ya hilo aliwataka wananchi kujenga mazoea ya kujenga nyumba imara na zenye ubora ili kuondokana na adha hiyo.
Aidha kwa mujibu wa Afisa maendeleo ya jamii wilayani humo Jabiry Ally alisema Kijiji cha Chalaminwe kilikumbwa na maafa kutokana na mvua iliyonyesha kwa wingi katika milima ya vijiji vya Singiwe na Chalaminwe mchana wa tarehe 16/02/2022 na kusababisha vifo kwa watoto wanne wa shule ya msingi Singiwe na nyumba nne kuharibiwa kabisa.
Alisema kufuatia tukio hilo Wataalam wa Halmashauri walifika eneo la tukio na kukutana na Uongozi wa Kata na Kijiji na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kiundinamema na Mambwekenya na kushauri ujenzi wa nyumba bora na kwa kutumia saruji.
‘’Pia watalamu walitoa elimu ya kupanda miti kuzunguka makazi yao ili kuzuia madhara ya vimbunga na upepo kwa kiasi kikubwa’’
Alisema kwa kutambua umuhimu wa watoto halmashauri ilitoa elimu kwa wazazi na walezi juu ya kuwalinda watoto ili kuwawezesha kukua katika mazingira bora ikiwemo kupata elimu stahiki.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.