Zikiwa zimesalia siku chache wanafunzi wa darasa la saba kuanza mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi,Mkuu wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura amewaagiza maafisa elimu wilayani humo kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi ambao watagundulika kuwashawishi watoto wao kufanya mitihani yao vibaya kwa lengo la kuwasaidia kazi za nyumbani.
Kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya wazazi na walezi wilayani humo kuwashawishi watoto wao kufanya vibaya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kwa lengo la kuwasaidia kufanya kazi za nyumbani zikiwemo kilimo,kuchunga ng’ombe na watoto wa kike kuwaozesha.
Hali hiyo imepelekea mkuu wa wilaya hiyo Julith Binyura Kuingilia kati swala hilo kwa kuitisha mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Matai na kuwataka wananchi kutoa taarifa za uwepo wa vitendo hivyo ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesema serikali haita wafumbia macho wazazi na walezi watakaokamatwa kwa tuhuma za kuwaachisha masomo watoto wao kwa kuwapeleka mashambani au machungani.
‘’kunatabia za baadhi ya wazazi ambao wana waambia watoto mkaandike vibaya vibaya sasa tutakaye mgundua ataenda jela akatumikie kifungo. Hivyo nimarufuku wazazi kuwaambia watoto mkaandike vibaya.
‘’Niwatake wanafunzi kutoa taarifa kwa walimu kama wazazi wenu watawashawishi kufanya mitihani vibaya. Niwatake pia wazazi muwaache wanafunzi wasome kwa amani na tuna imani mwaka huu wanafunzi wote watafaulu’’.alisema Binyura.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Efraim Moses Mwalemba, amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu sitahiki.
Amesema wazazi wanatakiwa kuwa na uelewa sahihi juu ya umuhimu wa elimu kwa kuwapeleka watoto wao shule kama Serikali ya awamu ya tano inavyotoa sera ya elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari
Hata hivyo kwa mwaka 2019 wanafunzi 3724 wilayani humo wanategemea kuanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi na huku mitihani hiyo ikitegemewa kuanza kufanyika Sptember 11 hadi 12 ,2019.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.