Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Julieth Binyura amewaweka ndani watu12 kwa muda usio julikana wakazi wa kijiji chaTatanda kata ya Sopa baada ya kufunga barabara kuu inayounganisha nchi ya Tanzania na Zambia kwa kuchimba mashimo na kuweka magogo sambamba na kusimika bendera zao katikati ya barabara hiyo na kupelekea msafara wake kukwama kwa muda.
Tukio hilo la kushangaza limetokea wakati mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura akielekea katika vijiji vilivyopo mpakani mwa nchi ya Zambia naTanzania kwa lengo la kutatua kero mbalimbali za wananchi ,ambapo akiwa katika maeneo ya kijiji cha Tatanda alikutana na vijana wapatao kumi na mbili wakiwa na majembe,panga na sururu wakiziba barabara kwa kuweka magogo.
Kufuatia hali hiyo alilazimika kuitisha gari ya jeshi la polisi wilaya humo na kuagiza kuwaweka ndani sambamba na kuwafunguilia kesi mahakamani ili iwefundisho kwa wengine wenye tabia chafu na ovu kama hiyo.
Akiongea mara baada ya kusitishwa kwa msafara huo,mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura,amesema kitendo hicho hakikubaliki kutokana na vijana hao kutaka kusababisha ajari na kusema kitendo cha wao kuweka bendera na kuchimba mashimo katikati ya barabara ni kosa kisheria.’
‘’kwanza kitendo walichokifanya cha kuzuia barabara kwa kuweka magogo ni kitendo kibaya kwani watu hawa tuwahesabu kama watu ambao walikuwa na nia mbaya ,kwani hapa gari yoyote ingepita kulikuwa nauwezekano mkubwa wa kuweza kupata ajari kutokana na magogo haya walio yaweka.’’alisema Binyura.
Amesema baada ya kukutana na hali hiyo msafara wake aliusitisha kwa muda na kuita gari ya polisi lengo likiwa ni kufanya mahojiano zaidi na vijana hao ilikujua nia yao ya kufanya hivyo.
‘’tumewakamata wote na watafunguliwa kesi mahakamani pamoja na kuhojiana nao zaidi kuwa ni kwanini waliamua kufanya kitendo kama hiki na wakati wameishi hapa miaka mingi na hakuna ajari mbaya ambazo zimewahi kutokea na kama zingekuwa zimetokea wangepaswa kutoa taarifa kwa viongozi husika ili kuwekewa matuta na sikama hivi walivyo fanya wao.’’alisema Binyura.
Aidha aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujichululia sheria mkononi na badara yake watoe taarifa kwa viongozi wa serikali za vijiji na kata pindi kunapokuwa kumetokea tatizo la aina yoyote kwa lengo la kuepukana na matatizo yasiokuwa ya lazima.
‘’sasa niwatake wananchi wangu muache tabia ya kujichukulia shera mkononi ikiwemo kuchimba barabara bila kuzingatia athari zake’’alisema Binyura.
Mtendaji wa kata hiyo JulisTete amelani vikali kitendo hicho na kusema kitendo hicho hakikubaliki na kuahidi kuendelea kuwalimisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara juu ya athari za kujichukulia sheria mikoni.
‘’kwanza kitendo hiki nakilani vikari tena kwa nguvu zote kwani kitendo walichokifanya wananchi wangu hakikubariki hata kidogo’’alisema Tete.
Hata hivyo imeelezwa kuwa wananchi hao walichimba barabra hiyo baada ya kuona mifugo yao ikiwemo nguruwe pamoja na kuku kugongwa na magari yanayofanya safari zake kutoka Kasesha mpakani mwanchi ya Tanzania na Zambia.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.