Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt.Lazaro Komba amezindua zoezi la uandikishaji orodha ya wapiga kura na kuwataka wandikishaji kuongeza umakini katika maeneo ya mipakani ili kuto andikisha watu kutoka nchi za jirani.
Zoezi hilo kwa ngazi ya wilaya limefanyika katika kijiji cha Matai ‘’B’’ na kusisitiza wananchi kundelea kujitokeza kujiandikisha ili kupata sifa za kuchagua viongozi wa serikali za mitaa Novemba 27/2024.
Msimamzi wa uchaguzi wilayani humo Shafi Mpenda, amesema uandikishaji huo ni kwa ajili ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji ambao utafanyika katika Vitongoji 422 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo na kusisitiza wananchi kuendelea kujiandikisha.
Hata hivyo Uandikishaji Wapiga kura unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti,Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za Mwaka 2024.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.