Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda amewataka wananchi kutembelea banda la Halmashauri hiyo ili kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo na ufugaji pamoja na kuona bidhaa mbalimbali zilizopo ikiwemo vipando vya mboga mboga na Rasilimali misitu.
Ameyasema hayo wakati wa maonesho ya nanenane ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya na kusisitiza wananchi kujitokeza kujifunza na kuona bidhaa mbalimbali kutokana na mwaka huu bidhaa kuwa nyingi ukilinganisha na mwaka uliopita.
Amesema kwa mwaka huu Halmashauri imefanikiwa kuboresha maeneo hayo kwa kiwango kikubwa ikiwemo kujenga jengo la maonesho kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.
Mapema akiongea wakati wa ukaguzi wa bidhaa mbalimbali kwenye banda la Halmashauri hiyo mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba akampongeza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kuongeza bidhaa za maonesho na kuwataka vijana na wananchi kujitokeza kwenye maonesho hayo ili kujifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.