Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Msongela Palela amezitaka kamati zote zinazohusika na maswala ya ukatili wa kijinsia kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji na kata katika kutokomeza mila potofu zilizojengeka katika jamii na kuwaagiza maafiasa maendeleo ya jamii kufuatilia na kutoa ripoti sahihi juu ya utekelezaji wa kazi hizo.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kamati za kupinga ukatili na mila potofu wilayani Kalambo mkoani hapa,ambapo amesema lengo la serikali ni kuhakikisha ukatili wa kijinsia na mila potofu zinatokomezwa katika jamii kwa kutoa elimu sitahiki kwa wananchi.
Amesema kamati hizo zitafanyakazi katika kata ishirini na tatu za wilaya hiyo na kuzitaka kamati hizo kuhakikisha elimu waliopatiwa inawafikia wananchi wote kwa muda muafaka.
‘’yale malengo tuliojiwekea ndio tukayatekeleze na mtakapo rudi katika vijiji na kata zenu nendeni mkawe walimu wazuri kwani hivi leo mmefundishwa ili mkawafundishe wengine’’.alisema Msongela.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Faustina Valeli amezitaka kamati hizo kufichua matukio ya ukatili wa kijinsia sambamba na kuwachukulia hatua kali wahusika wa matukio hayo kwa kuwafikisha kwenye vyombo vya dora kwa hatua zaidi za kisheria.
Mkurugezi kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Sukoda Samweli Mwazunga,amesema mradi huo utajikita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii juu na namna ya kuepuka ukatili wa kujinsia na Mila potofu katika jamii.
Mafunzo hayo yameshirikisha walimu wa shule za msingi na sekondari, Wahudumu wa afya vijijini (WAVI) , maafisa maendeleo ya jamii pamoja na watendaji .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.