Hali ya udumavu mkoani Rukwa imepungua kutoka asilimia 56.4 hadi kufikia asilimia 47.9 huku Halmashauri ya Kalambo ikitenga fedha kiasi cha shilingi million 60 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye hali hiyo.
Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alisaini mkata wa kukabiliana na afua za lishe na wakuu wa wilayani na kuzitaka Halimashauri zote kutenga fedha kiasi cha shilingi elfu moja kwa ajili ya watoto wenye afua za lishe.
Kwa kutekeleza hilo Halimashauri ya Kalambo imeanza utekelezaji wa mkakati huyo kwa utenga fedha kiasi cha shilingi million sitini huku msitizo ikiwa ni wadau wa lishe kutoa elimu kwa wananchi ili kuondokana na hali hiyo
Afisa lishe wilayani kalambo bwana Krispin, amesema wanaendelea na mkakati huo, ambapo kila baada ya miezi mitatu wanaka vikao na wajumbe wa kamati za lise ngazi ya wilaya kata na vijiji ili kabaini mapungupu yaliojitokeza kisha kuweka mpango mkakati.
Hivi karibuni vyombo vya habari na mashirika yasio ya kiserikali ikiwemo ECD yamekuwa msitari wa mbele katika kutoa elimu kwa wananchi ili kuhakikisha tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 linakwisha.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.