Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt Lazaro Komba amesema hali ya upatikanaji wa dawa muhimu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wilayani humo umefikia asilimia 84 ambapo jumla fedha shilingi 55,469,877.37 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 zimetumika kununua dawa,vifaa tiba na vitenganishi kutoka MSD hatua iliowezesha wananchi kupata huduma kwa urahisi.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bodi ya afya wilaya humo na kusema licha ya hilo serikali imepokea fedha kiasi cha shilingi 700,000,000/= kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na kwamba hadi kufikia juni 2025 jumla ya shilingi 83,624,453.92 zimetumika kwa jili ya ununuzi wa vifaa tiba kwenye zahanati.
Pamoja na mambo mengine ametumia fursa hiyo kuwataka wajumbe wa bodi ya afya wilayani humo kuwa mabalozi wazuri katika uzingatiaji wa sheria na miongozo ya serikali wakati wa usimamazi wa majukumu yao ikiwemo kusimamizi bajeti za vituo vya kutolea huduma za afya kwa kushirikisha jamii.
Mganga mkuu wa halmashauri hiyo Dkt Imanuel Mhanda amesema licha ya hilo vituo vya kutolea huduma za afya wilayani humo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 vimefanikiwa kukusanya fedha shilingi 45,406,016,.06 sawa na asilimia 67 kupitia vyanzo vyake vya makusanyo.
Hata hivyo Halmashauri imefanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wa bodi ya afya ambapo fauster ndaso amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa bodfi hiyo huku Endruw manyema ngindo akichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.