HALMASHAURI ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa inakabiliwa na upungufu wa watumishi 2,693 hali inayochangia wananchi kutopata huduma wanazotaka kwa muda muafaka.
Hayo yalibainishwa hivi karibuni na afisa mipango wa halmashauri hiyo,Eric Kayombo wakati akiwasilisha bajeti ya shilingi bilioni 36.4 kwanye baraza la madiwani wa halmashauri hiyo ambayo iliipitishwa na baraza hilo na itakuwa bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021.
Alisema kuwa halmsahauri hiyo inauoungufu mkubwa wa watumishi kitendo kinachosababisha baadhi ya huduma wanazohitaji wananchi kutozipata kwa wakati kutokana na upungufu huo.
Ofisa mipango huyo wa halmashauri hiyo alisema kuwa hali hiyo imetokana na baadhi ya watumishi kuondolewa kazini kutokanana na kuwa na vyeti bandia hivyo kupoteza sifa za kuwa watumishi wa umma.
Akiwasilisha bajeti hiyo, Kayombo alisema halmashauri hiyo katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 inategemea kutumia shilingi bilioni 27.0 kwaajili ya kulipa mishahara,shiringi bilioni 5.6 kwaajili ya miradi ya maendeleo, bilioni 1.8 kwaajili ya matumizi mengineyo.
"kwa upande wa makusanyo ya ndani halmashauri hiyo inatarajia kukusanya shilingi bilioni 1.8 kutokana na vyanzo vyake mbali mbali" alisema ofisa mipango huyo.
Baraza hilo liliipitisha bajeti hiyo kwa asilimia mia moja huku mwnyekiti wake Daudi Sichone akiwaasa wananchi kuona umuhimu wa kulipa Kodi na tozo mbalimbali ambazo zitawezesha kutekeleza miradi ya maendeleo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.