Watumishi wa umma katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kalambo wameadhimisha wiki ya utumishi kwa kufanya usafi kuzunguka maeneo ya soko la Santamaria huku kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Wambura Sunday akiwataka watumishi kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo ya serikali.
Awali akiongea na watumishi wilayani humo kupitia maadhimisho ya siku ya utumishi wa umma na utawala bora kaimu afisa utumishi wilayani humo Maria Leke amebainisha kuwa maadhimisho hayo ni moja ya matukio katika kalenda ya umoja wa Afrika (AU) ambapo kwa ngazi ya wilaya yamefanyika kwa kufanya shughuli za kijamii ikiwemo kufanya usafi maeneo ya soko sehemu za kutolea huduma za afya, kusikiliza na kutatua changamoto za watumishi kupitia vikao vya ndani pamoja na kusisitiza kutumia mifumo ya Kieletroniki kutoa huduma mbalimbali kama mfumo wa kujihudumia Watumishi (ess).
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wambura Sunday,amesema watumishi hawanabudi kuzingatia miongozo ya serikali ikiwemo kujiunga na mifumo ya TEHAMA inayo buniwa na serikali ili kurahisha utendaji kazi na kuepusha malalamiko.
Maadhimisho ya siku ya utumishi wa Umma hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 23 ya kila ifikapo mwezi wa sita ya kila mwaka ambapo kwa mwaka 2024 yameongozwa na kauli mbiu isemayo‘’kuwezesha kwa utumishi wa umma uliojikita kwa umma wa Afrika ya karne ya 21 iliyojumuishi na inayostawi ;ni safari ya mafunzo na mabadiliko ya Kiteknolojia’’.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.