Halmsahuari ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imeporomoka katika ukusanyaji mapato kwa anguko la asilimia 30% huku Halmashauri ya Kalambo ipanda kwa asilimia 46%.
Halmashauri hiyo imeteremka kimapato kutoka 66% mwaka jana kipindi kama hicho hadi kufikia 36.9% ambapo ni sawa na anguko la asilimia 30% ,
Hata hivyo kwa mujibu wa takwimu za mkoa ,Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa mwaka 2019 mwezi Februari makusanyo yalikuwa ni shilingi 1,517,348,839 sawa na 66% ya makadirio ya Shilingi 2,000,304,000 kwa mwaka 2020 hadi mwezi Januari, Halmashauri ya wilaya ya Nkasi ilikuwa imekusanya shilingi 919,830,000 .
Awali akiongea kupitia kikao cha baraza la madiwani wilayani humo ,Afisa wa Serikali za Mitaa wa Mkoa wa Rukwa Abinus Mgonya alisikitishwa kwa kuporomoka kwa ukusanyaji wa mapato ya Halamshauri hiyo hali ambayo ilikuwa tofauti ukilinganisha na mwaka wa fedha wa 2018/2019 katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi januari.
Alisema kuwa hali ya ulinganifu wa kipindi hicho siyo nzuri kwa Halmashauri ya Nkasi na kuongeza kuwa Halmashauri hiyo imekuwa ya mwisho kati ya Halmashauri nne za mkoa huo ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ikiongoza katika ukusanyaji wa mapato ikifuatiwa na halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, huku Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ikishika nafasi ya tatu.
“Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa mwaka 2019 mwezi Februari makusanyo yalikuwa ni shilingi 1,517,348,839 sawa na 66% ya makadirio ya Shilingi 2,000,304,000 kwa mwaka 2020 hadi mwezi Januari, halmashauri ya wilaya ya Nkasi ilikuwa imekusanya shilingi 919,830,000 na hii ni kwa mujibu wa takwimu tulizonazo pale mkoani kabla ya Halmashauri haijafanya usuluhishi wa mifumo ya matumizi na mifumo ya mapato ndio maana sisi pale mkoani inasomeka 36.9%,” Alisema
Manispaa ya Sumbawanga kwa mwaka 2019 mwezi Februari makusanyo yalikuwa shilingi bilioni 2.1 sawa na 98.1% ya makadirio ya shilingi bilioni 2.2 na Januari, 2020 imekusanya shilingi bilioni 1.7 sawa na 73% ya makadirio ya shilingi bilioni 2.4, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa mwezi Februari 2019 makusanyo yalikuwa shilingi milioni 801 sawa na 35% ya makadirio ya shilingi bilioni 2.3 na Januari 2020 imekusanya shilingi bilioni 1.3 sawa na 54% ya makadirio ya shilingi bilioni 2.3 na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa mwezi Februari 2019 makusanyo yalikuwa ni shilingi milioni 720.9 sawa na 36.05% ya makadirio ya shilingi bilioni 2. Na Januari 2020 imekusanya shilingi milioni 865.2 sawa na 46% ya makadiririo ya shilingi bilioni 1.8.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.