KATIKA jitihada za kutunza na kuhifadhi Mazingira, Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imeanza utaratibu maalumu wa kupanda miti katika maeneo tofauti ya wilaya hiyo na tayari imefanikiwa kupanda miti 1200 katika mji wa Matai.
Kaimu afisa mazingira wilayani humo Majanael Swalehe, alisema zoezi hilo litakuwa endelevu,ambapo wanatarajia kila jumamosi ya mwisho wa mwezi watakuwa wanapanda miti katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo ikiwa ni jitihada za kusaidia kutunza na kulinda mazingira ili yasiharibike.
"mpaka sasa tumefanikiwa kupanda miti 1200 na ili kuendeleza jitihada hizo tumeamua kuwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tutakua tunaendelea na kampeni hii na mwisho wa mwezi huu tutapanda miti katika eneo la hospitali ya wilaya" alisema ,Mjanaeli .
Hata hivyo siku ya Desember 8 ambayo ilikuwa siku ya kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika,wilaya ya kalambo ilitumia siku hiyo kupanda miti kuzunguka maeneo yote ya ofisi za Halmashauri ambapo viongozi mbali mbali wa wilaya walijitokeza kushiriki zoezi hilo.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Msongela Palela aliwataka wananchi kuwa na utaratibu wa kupanda miti katika maeneo yao ikiwa ni jitihada za kuzia upepo ili usiharibu makazi yao na huku katibu tawala wilaya hiyo, Frank Sichalwe aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.
‘’tunawapongeza wananchi kwa kujitokeza kwenu lakini ni vizuri mkawa na utaratibu wa kupanda miti katika maeneo ya makazi yenu ili kuhifadhi na kutunza mazingira.’’walisemaa viongozi hao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.