Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imefanikiwa kutekeleza mpango kabambe wa lishe wa taifa kwa kupunguza utapiamlo mkali kwa watoto chini ya miaka mitano
Utekelezaji wa mpango huo umekuwa ukitekelezwa na idara ya afya kwa kushirikina na idara mtambuka ambazo ni kilimo, elimu msingi na elimu sekondari kwa kutoa elimu ya lishe bora katika jamii kupitia vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye virutubishi.
Mapema akiongea kupitia kikao cha kamati ya lishe ya wilaya kilicho fanyika katika ukumbi wa mkuu wa wilaya hiyo Robert Tepeli, alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilifanikiwa kukagua vyakula na madini joto ikiwemo chumvi zinazo uzwa madukani sambamba na unyweshaji Vitamin (A) na kutoa dawa za minyoo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya.
Alisema katia kipindi hicho walifanikiwa kutekeleza zoezi la utoaji elimu kwa watoa huduma za Afya juu ya utambuzi wa utapiamlo na matibabu kulingana na hali ya utapiamlo.
‘’idara ya kilimo na mifugo inahusika moja kwa moja katika kutekeleza Afua za lishe kupitia kilimo na ufugaji ambapo katika kipindi hicho idara hiyo imefanikiwa kusimamia na kutoa elimu juu ya ufugaji bora wa samaki kwa wafugaji katika kata za Matai na Sundu na upandaji wa michikichi katika kata za Kasanga Mpombwe ili kuwezesha wananchi kunufaika na vitamin (A).’’alisema Tepeli.
Kwa upande wake kaimu afisa elimu msingi wilayani humo Nhand Jilala alisema idara hiyo imefanikiwa kutoa elimu na hamasa katika shule za msingi juu ya umuhimu wa wanafunzi kupata chakula shuleni angalau mlo moja kwa siku ikiwa ni pamoja na kufuatilia idadi ya shule ambazo zimekuwa zikitoa chakula kwa wanafunzi na kubaini shule 44 kati 99 kutoa huduma hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba alimwagiza afisa lishe wilayani humo kuhakikisha afua zote za zilishe zinatekelezwa ikiwa ni pamoja na kutenga fedha za utekelezaji.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.