Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere ameipongeza halmashauri ya Kalambo kwa kupata hati inayoridhisha kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo na kumtaka mkurugenzi mtendaji halmashauri hiyo Shafi Mpenda kuhakikisha fedha zote zinazo kusanywa zinawasilishwa benk kwa wakati
Ameyasema hayo kupitia kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ysa Kalambo kuhusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Kalambo, ambapo alipiga marufuku halmashauri kutumia fedha mbichi na kuagiza hatua dhidi ya watumishi waliotumia fedha mbichi na kufanya udanganyifu kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.
‘’Vilevile katika ufuatiliaji uliofanywa na mkoa umebaini kuwa yapo mapato katika mfumo wa LGRCIS yaliyokusanywa na watendaji wa halmashauri katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2023 kiasi cha shilingi 243,458,600 ambayo hayajawasilishwa benk hadi sasa .Nikuagize mkurugenzi kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa na wahusika wanachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa kuzingatia kanuni ya 36-37 ya kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2022’’. Alisema Makongoro.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Wambura Sundy, alisema kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 halmashauri imefanikiwa kukusanya fedha kiasi cha shilingi1,689,549,489 sawa na asilimia 83 huku kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ikifanikiwa kukusanya shilingi 1,710,607,360.41 sawa na asilimia 71 ya kiasi cha shilingi 2,412,405,000.000 ambacho kilikasimimiwa kukusanywa kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.