Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imepokea fedha kiasi cha shilingi 2,026,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata 16 za wilaya hiyo ikiwemo fedha za umaliziaji wa jengo la utawala shilingi 750,000,000 pamoja na fedha za umaliziaji jengo la mkurugenzi shilingi 50,000,000.
Miongoni mwa kata zitakazonufaika na fedha hizo ni pamoja na kata ya Mambwekenya ambayo imepata fedha kiasi cha shilingi 50,000,00 kwa ajili ya umaliziaji wa zahanati ya kijiji cha Kazonzya ,Mkowe shilingi 50,000,000 kwa ajili ya umaliziaji jengo la Zahanati ya Sengakalonje , Mwazye shilingi 50,000,000 kwa ajili ya umaliziaji jengo la Zahanati ya Mpenje, Mwimbi,shilingi 50,000,000 kwa ajili ya umaliziaji wa jengo la Zahanati ya kijiji cha Mozi , Ulumi shilingi 50,000,000 kwa kwajili ya umaliziaji wa jengo la zahanati ya kijiji cha Ulumi , Mambwenkoswe shilingi 50,000,000 kwa ajili ya umaliziaji jengo la Ilonga, Mpombwe shilingi 50,000,000 kwa ajili ya umaliziaji Zahanati ya kijiji cha Limba. Katete shilingi 50,000,000 kwa ajili ya umaliziaji Zahanati ya Jengeni.
Aidha katika swala la elimu msingi kata ya katete imepata fedha shilingi 40,000,000 kwa ajili ya umaliziaji wa shule ya msingi Katazi, 40,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 2 katika shule ya msingi Katazi ,Mabwekenya shilingi 40,000,000 kwa ajili ya umaliziaji madarasa mawili shule ya msingi , Mpombwe shilingi 40,000,000 kwa ajili ya umaliziaji madarasa mawili shule ya msingi Nondo, kata ya Msanzi shilingi 28,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 14 shule ya msingi katuka na shilingi 30,000,000 kwa ajili ya ujenzi ukuta wa bweni la shule msingi msanzi.
Licha ya hilo Kata ya Matai ni miongoni mwa kata zilizonufaika na fedha hizo kwa kupatiwa fedha shilingi 128,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa bweni shule ya msingi Matai ‘’A’’ shule na kata ya Katete ambayo imepatiwa fedha shilingi million 20,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa darasa moja la shule ya msingi Kaluko na kufanya jumla ya shilingi 366,000,000.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Kalambo Shafi Mpenda, amesema kata Ya Mkali imepata shilingi 60,000,000.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.