Halmashauri ya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa imesaini mkataba na kikundi cha M9 entertainment na kukabithiana pikipiki ya magurudumu matatu maalfu kama guta yenye thamani ya shilingi milioni sita na nusu ambayo itatumika kukusanya taka katika maeneo mbalimbali ya mji wa Matai.
Halmashauri ya wilaya ya kalambo inajumla ya vikundi vya ujasiliamali 492 na huku vikundi 58 vikiwa vimekopeshwa fedha na halmashauri hiyo na vikundi kumi na tano vikiwa kwenye mkakati wa kupatiwa mikopo.
Akiongea mara baada ya kusaini mkataba na kikundi hicho afisa mazingira wilayani humo Adam Baleche,alisema kutokana na halmashauri hiyo kutokuwa na gari ya kuzolea taka hivyo ililazimika kununua pikipiki ya magurumu matatu malfu kama Guta na kukikopesa kikundi cha M9 ENTERTAINMENT kwa lengo kusaidia kuzolea taka katika kata za lyowa na Matai
‘’Halmashauri baada ya kukosa gari ikaona ni bora inunue pikipiki ya magurumu matatu ambayo yumewakopesha vijana wa kikundicha M9 entertainment na kusainiana mkataba na lengoni kuhakikisha wazoa taka kwenye maeneo yote yanayo unda mji wa Matai na kutupa dampo huko Matai Asilia.’’alisema Baleche’’
Mwenyekiti wa kikundi hicho Musa Mzopora.alisema licha ya chombo hicho kuwa saidia kutoa taka pia kitawasaidia kujipatia kipato.
‘’leo tumekutana hapa ili kusainiana mkataba baina yetu na halmashauri na kama unavyo ona hata ukipita kwenye maeneo ya masoko na barabarani utakuta taka zimezagaa ,hivyo naona hii itasaidia kwa kiasi kikubwa hususani katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko kamavile kipindupindu.’’alisema Mzopora.
Siku za hihi karibu mkuu wa wilaya Julieth Binyura aliagiza jeshi la polis kuwakama na kuwaweka ndani kwaa muda wa saa 48 mtu au watu ambao wataonekana wakitupa taka ovyo kwenye maeneo ya mji huo.
‘’yule ambae atakutwa maeneo yake ni machafu atakamatwa na kuwekwa ndani kwa saa arobaini na nane ,kwahiyo ndugu zangu kuweni wasafi kutokana na kuwa huu ni mji ‘’alisema Binyura.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.