Hatimaye Wananchi Wahamasika Na ujezi Wa Kituo Cha Afya Samazi
Posted on: July 1st, 2019
Siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachimu Wanagabo kuingilia kati mgogoro wa wa ujenzi wa kituo cha afya Samazi wilayani Kalamb ,hatimaye wanaanachi kwenye maeneo hayo wamenza ujezi wa kituo hicho na kushiriki shiriki shughuri za maendeleo.
Akiongea kwa niaba ya wananchi waishio katika eneo hilo, Afisa mtendaji kata ya Samazi ndugu Pius Joachim Kasonso alisema tangu walipo pata taarifa ya maandishi kuhusu mradi huo walitoa elimu kwa wananchi juu ya manufaa ya uwepo wa kituo cha afya na kwamba tayari wamesha anza kusafisha la ujenzi wa mradi, kuchimba mawe na kusomba mchanga vitendo vinavyoashiria kuanza kwa ujenzi .
Naye Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ndugu Anatorius Nobe Mwikala alisema uwepo wa kituo cha afyaSamazi utapunguza kwa kiasi kikubwa adha kwa wananchi kufuata huduma za afya Ngorotwa, Matai na Sumbawanga kama ilivyo hivi sasa.
Akithibitisha uwepo wa mradi huo,Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya ya Kalambo ndugu Daudi Sebinga alisema Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo imepokea jumla ya shilingi milioni mia nne kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Samazi.
``Mradi wa kituo cha afya Samazi utahudumia vijiji vya Samazi, Kisale,Kipanga na Katili vyote vikiwa ndani ya kata ya Samazi pamoja vijiji jirani vya Kafukoka, Kachele na visiwa vya karibu vilivyomo ndani ya mwambao wa ziwa Tanganyika.
``Majengo yatakayojengwa kwenye hii awamu ni pamoja na jengo la Mama na mwana,wagonjwa wa nnje[OPD],Maabara,Upasuaji na Utawala ambayo yote kwa pamoja yatagharimu kiasi cha milioni mia nne za kitanzania.’’
Mhandisi Daudi Sebinga aliwataka wananchi kuendelea kujitolea nguvu kazi ili kupunguza gharama kwani fedha zilizotolewa na serikali kuu hazitoshi kukamilisha ujenzi wa mradi huo.