Marehemu Costansia Gasto Nyembele alizaliwa tarehe 23/09/1961 katika Kijiji cha Mwimbi, Kata ya Mwimbi, Wilaya ya Kalambo na kubatizwa tarehe 26/09/1961 na kupata komunio mwaka 1972 na mwaka1978 alipata kipaimara Katika Kanisa la Yakobo Parokia ya Ulumi. (Roman Catholic) na kuhitimu shule ya Msingi Kalambo mwaka1977.
Marehemu aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Mwimbi, mjumbe baraza la kata ya Mwimbi,mzee wa baraza la mahakama ya Mwimbi na mjumbe wa bodi ya shule ya sekondari Mwimbi na baadae alichjaguliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Mwimbi na badae kuwa diwani wa tarafa hiyo.
Hata hivyo katika maisha ya kisiasa, Mwaka1985 marehemu alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya ya Sumbawanga kabla ya Wilaya ya Kalambo Haijaanzishwa. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mwaka1995 alichaguliwa kuwa Diwani Viti Maalum Tarafa ya Mwimbi na kutumikia nafasi hiyo kwa vipindi tofauti hadi ilipoanzishwa Wilaya ya Kalambo.
Aidha Mwaka 2013 Wilaya na Sumbawanga iligawanywa na kuzaliwa Wilaya ya Kalambo, ambapo marehemu alikuwa katika nafasi hiyo ya Udiwani wa Viti Maalum Tarafa ya Mwimbi. Nafasi ambayo ametumikia kwa vipindi vitatu hadi umauti wake. Akiwa katika nafasi ya udiwani alitumikia katika kamati mbali mbali za kudumu za Halmashauri akiwa kama mjumbe Kamati ya fedha, uongozi na mipango kwa vipindi vinne, 2015/2016, 2016/2017, 2020/2021 na 2021/2022, Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira kwa vipindi nane, 2013/20214, 2014/2015, 2017/18, 2018/2019, 2019/20, 2022/2023 na 2023/2024 hadi umauti ulipomkuta alikuwa mjumbe wa kamati hiyo.
Aidha Marehemu Costansia alikuwa na matatizo ya Moyo yaliyogunduliwa mwaka 2019 katika Hospitali ya watu wa Korea Kibaha- Pwani, alikuwa akitibiwa katika Hosptali mbali mbali za Kristu Mfalume (Dr. Hatman), Kituo cha Afya Mwimbi, Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, Hospital ya Alfa-Dar es Salam na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Hata hivyo, mnamo tarehe 23/03/2024 hali ya Mgonjwa ilibadilika na kukimbizwa katika Kituo cha Afya Mwimbi na kupatiwa matibabu ya dharula ambapo Madaktari walijitahidi kuokoa maisha lakini aliaga Dunia. Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 63.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.