Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imepokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 674,524,662.74 kutoka ofisi ya Rais TAMISEM ikiwemo vifaa vya upasuaji, mashine za kutunza watoto njiti, X-RAY na vifaa vya macho ambavyo awali vilikuwa vikipatikana katika hospitali ya rufaa ya kanda jijini Mbeya.
Mapema akiongea wakati wa ukaguzi wa vifaa hivyo mratibu wa vifaa tiba wilayani humo Mhandisi Bane Matari amesema vifaa hivyo vinajumuisha vitanda 60, vifaa vya uchunguzi na vifaa kwa ajili ya matibabu na vifaa vya upasuaji kwa akina mama wajawazito.
Amesema licha ya hilo hospitali imepokea mashine ya kisasa ya X-RAY (digtal X-RAY mashine,Utrasound mashine ambavyo tayari vimeshafungwa kwa ajili ya matumizi.
Amesema katika mwaka wa fedha 2022 /2023 serikali ilipokea fedha za Ruzuku toka serikali kuu,kiasi cha shilingi 100,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vya huduma za meno na macho ambavyo tayari vimefungwa na kuanza kutoa huduma.
Kwa upande Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo Emmanuel Kisyombe amesema hospitali hiyo inapokea wagonjwa 700 hadi 800 kwa mwezi na kwamba kwa kipindi cha kuanzia mwezi septemba wamepokea wagonjwa 800 kati yao wanawake wanaojifungua wakiwa 50 na kufanya upasuaji kwa wanawake 5.
Hata hivyo halmashauri ya Kalambo kwa mwaka wa fedha 2020/202 3 ilipokea fedha 3,440,000,00 kwa ajili ya ujenzi wa majengo 7 ikiwemo jengo la maabara, jengo la utawala, jengo la wagonjwa wa nje (OPD) Jengo la wazazi (martenity ward) jengo la mionzi (Radiologia,Jengo la kufulia (laundry) na jengo la kuhifadhia dawa (Pharmacy) na kwamba wodi tatu ikiwemo ya watoto , wodi ya wanawake na wodi ya wanaume zimekamilika na kuanza kutoa huduma.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.