Wagonjwa wengine sita wa virusi vya corona wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo kisiwani Zanzibar. Hatua hiyo inafanya idadi ya wagonjwa wa virusi hivyo kupanda kutoka watu 18 hadi 24.
Waziri wa Afya kisiwani humo Hamad Rashid Mohamed amesema kwamba wagonjwa wote ni raia wa Tanzania na hawana historia ya kusafiri .
Waziri huyo ameongezea kwamba tayari wagonjwa wote wamelazwa katika vituo maalum kwa lengo la kuendelea kupata matibabu.
Serikali ya kisiwa hicho imeendelea kuwasisitizia wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo zinazotolewa mara kwa mara ikiwemo kunawa mikono.
Wizara ya Afya kisiwani vilevile imewaomba wananchi wenye dalili za homa kali , kukohowa na kupiga chafya kujitokeaza katika vituo vya Afya.
Aidha raia kisiwani humo wametakiwa kuchukua tahadhari wakati wanapowazika watu waliofariki kutokana na virusi hivyo ili kuzuia maambukizi zaidi.
Tangazo hilo linajiri saa 24 baada ya taifa la Tanzania kutangaza wagonjwa 29 wapya wa virusi hivyo nchini humo.
Akithibitisha hilo waziri wa Afya Ummi Mwalimu alisema kwamba wagonjwa 26 kati yao wapo katika mji wa Dar es Salaam huko wawili wakipatikana mjini Mwanza na mmoja akiwa katika eneo la Kilimanjaro.
Hatahivyo waziri huyo pia alitangaza habari njema akisema kwamba hadi kufikia Jumatano takriban watu 11 walikuwa wameshapona virusi hivyo lakini akaongezea kwamba watu wanne walifariki.
Ongezeko hilo la wagonjwa linajumlisha wagonjwa wapya sita waliotangazwa na waziri wa Afya wa kisiwa cha Zanzibar.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.