Wananchi mkoani Rukwa wameipongeza serikali kwa kuendelea kusimamia swala la watu kunawa mikono yao kwa kutumia mitambo ya kisasa ambayo ilibuniwa na chuo cha MUSTI Mbeya na Rukwa hivi karibuni kwa nia ya kuwakinga na covid 19.
Katika nyakati tofauti wananchi hao wamesema serikali haina budi kuendelea na jitihada za kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kunawa mikono licha ya ugonjwa wa covidi kuripotiwa kuisha nchini hapa .
Kaimu mganga mkuu wilayani kalambo Dr .Chuki,alisema serikali kupitia idara ya afya bado inaendelea na jitihada za kuhamasisha wananchi kupitia makongamano, mikutano ya hadhara na washa mbalimbali juu ya umuhimu wa kujikinga na magonjwa hayo.
Awali akizindua mitambo hiyo mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo, alisema kila mwananchi hana budi kujikinga na ugonjwa huo kwa kujenga mazoea ya kunawa mara kwa mara mikono kwa kutumia sabuni na maji safi.
Hivi karibuni mashirika binafisi ikiwemo ECD yamekuwa msitari wa mbele katika kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kunawa mikono kila wakati.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.