Tume huru ya uchaguzi nchini imeanza kutoa mafunzo ya namna bora ya ujazaji wa fomu kwa kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (voters) REGISTRATION SYSTEM –VRS) pamoja na matumizi ya vifaa vya uandikishaji wapiga kura huku ikiwataka waandikishaji wasaidizi wa kata kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na tume ili kufanikisha zoezi hilo la kitaifa.
Awali akifungua semina ya mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata wilayani Kalambo mkoani Rukwa, afisa uandikishaji Jimbo la Kalambo ndugu Erasto Mwasanga, amesisitiza waandikishaji wote kuhakikisha wanavitunza vifaa vitakavyo tumika katika uboreshaji kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na tume ili kuwezesha kufanya kazi kwa usahihi.
Licha ya hilo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uboreshaji wa taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa maendeleo ya wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla na kusema zoezi la uandikishaji litahusisha waandikishaji wapya na uboreshaji wa taarifa za wapiga kura.
‘’tunatarajia kuwa baada ya mafunzo haya nyie pia mtapaswa kutoa mafunzo mliopata hapa kwa waendeshaji wa vifaa vya bayometriki na waandishi ambao watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni ‘’ alisema Mwasanga.
Awali akiongea na wadau mkoani Rukwa mwakilishi wa mkurugenzi wa tume ya uchaguzi nchini Martin Mnyenyelwa amesema uboreshaji wa daftari unalenga kuwaandikisha raia wa Tanzania waliotimiza umri wa miaka 18 na zaidi au watakao timiza umri huo wakati wa tarehe ya uchaguzi wa mwaka 2025 na ambao hawajapoteza sifa kwa mujibu wa Sheria ya uchaguzi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.