JAJI mkuu wa Tanzania Prof,Ibrahimu Juma amesifu mahusiano mazuri
yaliyopo kati ya Mahakama na serikali wilayani Kalambo na kuwa ajenda kubwa kwa mahakama ni kujenga mahusiano mema na Mihimili mingine ya dola kwani wote wanategemeana.
Amesema kuwa taarifa iliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura inaonyesha kuwa mahusiano yaliyopo kati ya mahakama na serikali ni mazuri kiasi kwamba hata utendaji kazi wa shughuli za mahakama unakua rahisi.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na na kamati ya ulinzi na usalaama ya wilaya ya kalambo wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kutembelea na kukagua utendaji wa mahakama katika wilaya zote tatu za mkoa huo.
Amesema kuwa mahakama pekee haiwezi kufanikisha kazi zake kwa ufanisi bila ya kujenga mahusiano mazuri na wadau wengine na kuwa hata ziara yake anayoifanya lengo lake kuu ni kuonana na wadau na kujenga mahusiano mazuri .
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura amesema wanajitahidi kuongea na wananchi kupitia mikutano ya hadhara kwa lengo kumaliza migogoro kabla ya kufikishwa mahakamani.
Katika hatua nyingine akiwa katika wilaya ya Nkasi jaji mkuu wa Tanzania alisema kuwa mahakama inaangalia uwezekano wa kuanza utaratibu wa kutoa nakala za hukumu kwa lugha ya kiswahili ili kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa haki katika vyombo vyake vya maamuzi.
Alisema kuwa hoja ya mahakama kutoa nakala za hukumu kwa lugha ya kiswahili ni jambo la msingi na litasaidia upatikanaji wa haki kwa wananchi wanaofika mahakamani kutafuta haki juu ya mashauri mbalimbali.
Alisema pia itawasaidia kufahamu na kuelewa kwa urahisi kile kilichoamuliwa na mahakama, hivyo yule anayetaka kukata rufaa mahakama ya juu inakuwa rahisi kwake kufanya hivyo na kwa wakati sahihi.
"Hii hoja ya kutumia lugha ya kiswahili katika mahakama zetu ni jambo la msingi na muhimu sana.....tumeipokea na tutaifanyia kazi" alisema
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.