Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amesema wanafunzi 282 kati ya 302 wa memkwa waliofanya mitihani ya kitaifa ya upimaji wa darasa la nne kwa mwaka 2023 wamefanikiwa kujiunga na mfumo rasim wa masomo huku wanafunzi 1785 wakiwemo wavulana 899 na wasichana 886 wamefanikiwa kujiunga na madarasa ya Memkwa katoka halmashauri nne za mkoa huo.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya kilele cha elimu ya watu wazima yaliofanyika wilayani Kalambo kwa ngazi ya mkoa na kuwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Kalambo Dkt.Lazaro Komba ambae amesisistiza jamii kujiendeleza kielimu kwa kujiunga na elimu ya watu wazima ikiwa ni pamoja na shule zote mkoani humo kuwa na vyumba maalum kwa ajili ya watu wazima kujiendeleza.
Aidha amesema Matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 inaonesha 25.9% ya Watu wazima hawajui Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) na kwamba kupitia takwimu hizo ni dhahiri kuwa changamoto ya Wananchi kutojua KKK ni kubwa hivyo Wazazi na walezi wanajukumu kubwa la kutimiza majukumu yao ya ulezi na kuhakikisha watoto wao wahudhuria masomo katika mfumo rasmi wa Elimu.
Kwa Upande wake Kaimu Afisa Elimu Mkoani humo Matinda Mwinuka amesema ukosefu wa vitendea kazi maalumu kwa ajili ya watu wazima na mwamko duni wa vijana kujiunga na vyuo vya elimu ya watu wazima ni miongoni mwa changamoto ambazo walimu wamekuwa wakikabilina nazo wakati wa kutoa elimu hiyo.
Baadhi ya wadau wa elimu mkoani humo akiwemo Erick Skale wamesema serikali haina budi kuwekeza katika elimu ya watu wazima kwa kuboresha mindombinu na kuongeza vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji ili kuwesha kufikia malengo yao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.