Mwanasheria wa Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa Peter Malendecha amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kuandika wosia ili kuepuka migogoro ya kifamilia na kijamii ambayo wakati mwingine imekuwa ikijitokeza pindi ndugu jamaa na marafiki wanapofariki.
Ameyasema hayo kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia inayofanyika katika kata 10 za wilaya hiyo na kusisitiza jamii kuzingatia umihimu wa kuandaa wosia kwa kuzingatia uwepo wa mashahidi maalumu wasio pungua wanne.
Kwa upande wake mratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria kutoka wizara ya Katiba na sheria Doreen Mhina ametumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilayani humo kuwa sehemu ya kupinga na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pindi matukio hayo yanapojitokeza.
Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia inafanyika katika halmashauri nne za mkoa wa Rukwa ambapo kwa wilaya ya Kalambo inafanyika katika kata 10 kwa kutoa elimu kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.