Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imeanzisha kampeni ya chanjo ya mifugo aina ya ng’ombe ili kuikinga mifugo hiyo dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika kijiji cha Katuka katibu tawala wilayani humo Servin Ndumbalo,amesema utolewaji wa chanjo hiyo itasaidia kukinga mifugo dhidi ya vimelea mbalimbali vya magonjwa kama homa ya mapafu.
Aidha amewataka wafugaji kuzingatia chanjo kwani zinaweza kusaidia kuwapunguzia gharana za matibabu,kuepusha vifo vya mifugo, sambamba na kusaidia kuongeza upatikanaji wa mazao yanayotokana na mifugo ikiwemo nyama na maziwa ambayo yamekuwa yakisaidia kuboresha afya za binadamu
Kwa upande wake daktari wa mifugo kutoka wizara ya mifugo na uvuvi Dkt Rajabu Mkwela,amesema serikali inakusudia kuchukua sampuli pamoja na kupata historia ya mifugo ilio kumbwa na magojwa ya kwato na upofu wa macho katika vijiji vya kata ya Mbuluma na Msanzi wilayani humo.
Baadhi ya wafugaji wilayani humo ambao licha ya kuipongeza serikali kwa kuanzisha kampeni ya chanjo wilayani humo ,wakaishauri serikali kuona uwezekano wa kutafuta chanjo ya ugonjwa wa kwato na upofu wa macho.
Mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi wilayani humo Nichoraus Mlango amesema wilaya ya Kalambo ina mifugo ya aina mbalimbali ikiwemo ng’ombe wapatao 221,456, Mbuzi 38,475, Kondoo 12,482, Punda 2,795, Mbwa 6,882, Nguruwe 7,442, kuku 166,332 na kwamba katika kuwawezesha wafugaji kiuchumi wameazisha chanjo ambayo itatolewa katika vijiji tofauti vya wilaya hiyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.