Msimamizi wa fedha kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa Mpapalika Mfaume ameipongeza halmshauri ya Kalambo kwa kufanikiwa kununua mashine 128 za ukusanyaji mapato kwa mfumo wa Tausi ambazo zitasaidia kudhibiti wadaiwa sugu wa mapato (Defaulters) na kuboresha hali ya ukusanyaji wa mapato.
Ameyasema hayo baada ya kufanya ziara ya kutembelea halmashauri za mkoa huo ikiwemo halmshauri ya Kalambo na Nkasi ili kuona muenendo wa utekelezaji wa agizo la serikali la matumizi sahihi ya mashine za mfumo wa Tuusi. Ambapo amesema kuanzia kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 mkoa wa Rukwa umefanikiwa kukusanya fedha billion 3,000,000,000/= sawa na asilimia 30 na kwamba kati ya hizo Halmashauri ya Kalambo imefanikiwa kukusanya shilingi 734,672,000/= sawa na asilimia 30.
Hata hivyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 halmashauri ya Kalambo inatarajia kukusanya fedha shilingi billion 2,412,405,000 huku katika swala la ununuzi wa mashine za ukusanyaji mapato kwa mfumo wa Tausi ikifikia asilimia 99 ukilinganisha na halmashauri zingine za mkoa huo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.