Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imepata makombe 12 baada ya kuibuka na ushindi katika mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA ambayo yalikuwa yakifanyika kitafa mkoani Tabora na kuwa Halmshauri ya kwanza kwa ngazi ya mkoa katika michezo ya Jumla huku wazazi na walezi mkoani humo wakitakiwa kuwarushu watoto wao kushiriki kikamilifu kwenye michezo hiyo ili kuimalisha afya na uwezo wa masomo darasani.
Akipokea makombe hayo,mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda aliwapongeza walimu wa michezo wilayani humo kwa kuibuka na ushindi huo na kumwagiza mkuu wa kitengo cha michezo wilayani humo Amos Mmewa kuhakikisha kila shule inakuwa na vifaa vya michezo pamoja na kuboresha viwanja vya michezo ili kuwezesha wanafunzi kupata sehemu rafiki ya kufanyia michezo.
Kwa upande wake afisa utumishi na utawala wilayani humo Amandus Mtani aliwataka wazazi na walezi wilayani humo kuwaruhusu watoto kushiriki kikamilifu kwenye michezo hiyo ili kuimalisha afya na kuendeleza vipaji vyao kutokana na kwamba michezo ni ajira.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.